๐๐ ๐๐๐๐๐๐ (๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐)
๐๐จ๐ฎ ๐๐ซ๐ ๐๐ฅ๐ฅ๐จ๐ฐ๐๐ ๐ญ๐จ ๐๐จ๐ฉ๐ฒ ๐ญ๐ก๐ ๐ฌ๐ญ๐ซ๐ฎ๐๐ญ๐ฎ๐ซ๐ ๐๐ฎ๐ญ ๐ง๐จ๐ญ ๐๐จ๐ฉ๐ฒ๐ข๐ง๐ ๐๐ง๐ ๐ฉ๐๐ฌ๐ญ๐ข๐ง๐ ๐ฌ๐จ๐ฆ๐๐ฐ๐ก๐๐ซ๐. ๐๐ก๐ข๐ฌ ๐ข๐ฌ ๐ ๐ฉ๐๐ซ๐ฌ๐จ๐ง๐๐ฅ ๐๐จ๐.
๐๐๐๐๐ง๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ก๐๐๐ 2016
This picture is unavailable now
๐ญ๐จ๐ฎ๐๐ก ๐ญ๐ก๐ ๐ฅ๐ข๐ง๐ค ๐๐๐ฅ๐ฅ๐จ๐ฐ ๐ญ๐จ ๐๐๐๐๐ฌ๐ฌ.
๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐
๐๐ ๐๐๐
๐
HISTORIA YA MAISHA YANGU
Mtunzi: R. M. Omary
Mhariri: Z. B. Ibrahim
Copyright reserved © 2019
Abdulrahman Alsumait
(SUMAIT) University.
Utangulizi mfupi
Ndugu msomaji wa kitabu hiki cha HISTORIA YA MAISHA YANGU, natumain utapata faida za kutosha katika kukisoma kitabu hiki, kwani ndani yake kuna changamoto na mafanikio makubwa yanayoweza kubadili maono ya mtu hasa yule aliyekata tama katika Maisha yake.
Mwandishi wa kitabu hiki ni mimi Ramadhani Mustafa Omary, ambaye ndio mhusika wa historia hii iliyopo ndani ya kitabu hiki.
Historia hii sio ya kutunga bali ni maisha ya kweli niliyoishi mimi na wote wahusika waliokuwemo ndani ya historia hii.
HISTORIA YA MAISHA YANGU
Uzawa
Nimezaliwa katika Kijiji Cha Zigha Randan, kata ya Malindi jimbo la Mlalo, Wilaya ya Lushoto jijiini Tanga, tarehe 24 mwezi wa 7 mwaka 1994 Miladia, siku ya jumapili, sawa na tarehe 15 mwezi wa pili (Swaffar) mwaka 1415 Hijiria.
Tulizaliwa watoto nane kwa mama mmoja ambapo watatu wameshatangulia mbele ya haki na kubakia watano ambao ni Ashirunah, Ramadhan, Khalfan, Nasri na Ashura. Baada ya miaka mingi kidogo baba yetu alioa mke wa pili na kupata motto mmoja wa kiume aliyeitwa Ali.
Baada ya mimi kuzaliwa katika mwaka huo 1994 nilikaa na wazazi wangu kijijini kwa muda wa takriban miaka mitano na kusafiri na baba yangu mdogo aliyeitwa Yasini kwa ajili ya kwenda kuishi naye katika jiji la Dar es Salaam ambapo alikua na Mke na mtoto mmoja tu aliyeitwa Asha. Nilikaa Dar es Salaam kwa muda kisha nilitamani na kulilia kurudi kwa wazazi wangu kijijini Zigha Randan. Baada ya baba mdogo na mkewe kushindwa kuzuilia kilio changu cha kutaka kurudi kijijini kwa wazazi wangu, waliamua kunirejesha ambapo furaha yangu ilipatikana kwa kuonana kupya na mama yangu mzazi kwa sababu yeye ndiye niliyemkosa mda mrefu kwani baba alikua akija Dar es Salaam kunitembelea anapokua na safari zake za kibiashara.
Ndoto za baba yetu
Baba yetu alikua na ndoto za kuishi jijini Dar es Salaam yeye pamoja na familia yake kama ambavyo baadhi ya wadogo zake walifanikiwa katika ndoto hiyo. Ndoto zake hizi zilikwamishwa na bwana mmoja aliyeitwa Salehe ambaye alikua ni rafiki wa baba wa karibu sana. Ilikua ni baada ya kulewa pombe ambapo mlevi huyo alimvamia baba na kutaka kuchukua mali zake na hapo ndipo walipigana. Kwa bahati mbaya baba yeye hakujiandaa kwa vita hiyo na hali adui wake alikua na silaha ambazo ni Rungu na Panga lililojaa kutu. Baada ya baba yetu kuzidiwa kwa kujeruhiwa sana sehemu za kichwani, mguuni na begani, alipoteza fahamu na kuzinduka baada ya kiasi cha takriban wiki moja akiwa yuko hospitali kuu ya taifa ya muhimbili. Katika kipindi chote hiki familia yake ilikua kijijini kwani yeye alienda kutafuta maisha ili aihamishe familia yake iliyokua katika hali duni huko kijijini. Akina mama na bibi mzaa baba walisafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kumwona baba aliyekua akipumulia mitungi ya oxygen gas katika chumba cha ICU. Baada ya kupata nafuu na kuruhusiwa kutoka hospitali baba alirejea kijijini na kuendeleza maisha yake hukohuko. Adui wake Salehe ambaye alikimbia kwa kesi ya kumdhuru rafiki yake, alikuja kuugua na kufariki dunia.
Hapo ndipo zilipoishia ndoto za baba yetu za kuishi Dar es Salaam kwani kuanza upya kulikua ni jambo gumu sana inagawa hakukata tamaa. Sababu zilizomrejesha nyuma ni kufifia kwa juhudi zake kutokana na athari za majeraha aliyokua nayo mwilini mwake.
Kuanza kwangu shule
Ilipofika mwaka 2001 baba aliniandikisha chekechea ambapo mwanzo tulisomea katika kanisa la Mtumbi kwani mwalimu alikua ni mchungaji wa dini ya kikristo. Baada ya muda tulihamia Shule ya Msingi Zigha ambapo nilimaliza chekechea na kuanza kusoma darasa la kwanza.
Uhalisia wa jina langu ilikua niitwe Aboubakar kwani ndio jina nililopewa na baba lakini wengine walipenda kuniita jina la babu mzaa mama ambalo lilizoeleka sana kiasi cha kumpa baba ugumu katika kuchagua ni jina gani aniandikishe shuleni. Mwisho baba aliamua kuandika lile ambalo lilizoeleka na hata mimi pia nilishalizoea nalo ni Ramadhan.
Nilianza rasmi darasa la kwanza mwaka 2002 nikiwa na umri wa miaka saba. Kuanzia darasa la kwanza mpaka la tatu sikua najielewa kwani nilikua sijitumi kama mwanafunzi na kufeli au kufaulu kwa bahati kuliwa ni jambo la kawaida kwangu. Baada ya kufika darasa la nne hapo ndipo mambo yalibadilika kwani tulitangaziwa kubaki darasa la nne ikiwa hatutofaulu vizuri kwenda darasa la tano. Nlijitahidi na kua katika nafasi nzuri japo sikuweza kuongoza darasa. Kipindi hicho ambacho kulikua na mwalimu mpya wa kiingereza aliyeitwa John, alinipenda sana kwa juhudi yangu hasa kwa mara ya kwanza alipotaka tuzitambue pesa kwa kuzitaja kiingereza jambo ambalo alikua akinifundisha babaangu kwa njia tofauti tukiwa nyumbani.
Baba yetu hakurudi nyuma katika kutusisitiza kujitahidi katika kila upande wa mafanikio ikiwemo kusoma kwa bidii, kuhudhuria madrasa kwenda shambani, kutafuta majani ya ng’ombe na watu wa aina zote.
Ilikua ni familia yenye upendo na utulivu wa hali kuheshimu ya juu kwani baba hakuruhusu utovu wa adabu hata kidogo.
Wakati tunafanya mtihani wa darasa la nne wa kiingereza nikiwa na fikra za kua mimi bado mdogo, hivyo nikifeli nitarudia tu, hapo alipita msimamizi wa mtihani ambaye hakua ananijua nasi wala hatukumjua, alivyoangalia mwandiko wangu na kuuona mzuri wenye mpangilio mzuri, nayo ilikua ni imla (Dictation) ya kiingereza tuliyosomoewa, Yule msimamizi alimwambia mwenzake mbele yangu “Namna hii mtoto asifaulu”? nikapata furaha japo najua yeye sio msahihishaji na kiukweli tulitishiwa vya kutosha kwani tulifikia kuambiwa kua mitihani ya darasa la nne inasahihishwa kwa computer na hivyo ukifutafuta tu basi mtihani wako hautopita kwenye computer. Kwa uhalisi hakuna aliyewahi hata kuiona hiyo computer miongoni mwetu kipindi hicho na wala hatukuelewa ni kitu gani bali tulijua ni mtambo maalumu wa kusahihishia mitihani.
Matokeo yakaja na kusomwa majina ya waliofaulu na waliorudia. Nilifurahia kua miongoni mwa waliofaulu kwenda darasa la tano kwani waliofeli walizomewa na kujisikia vibaya sana.
Kuanzia hapo nikawa najitahidi sana kusoma yale masomo niliyoyapenda na tangu nipo mdogo nilikua nikiulizwa unataka kua nani basi hujibu nataka kua Doctor pamoja na kua sikujua masomo gani yananedana na fani hiyo.
Nilitamani sana kua Doctor kwani niliwaonea huruma wagonjwa kila nilipokwenda hospitali na kuona waliopatwa na ajali na waliolazwa kwa magonjwa tofautitofauti.
Nilisoma sana sayansi, hesabu, stadi za kazi na kiingereza. Nilichukia sana somo la marifa ya jamii kwani nilikua nikiona sielewielewi habari za vita za dunia na matukio ya kihistoria. Hata hivyo nilijitahidi kufaulu masomo hayo.
Baba alikua akinifungia chumbani kwake usiku kabla ya chakula cha jioni ili nijisomee. Kwa bahati mbaya kutokana na akili zangu niliona sina cha kusoma kwani tangu nipo darasa la sita nilikua ni wa kwanza au wa pili. Watu ambawo walikua wakichuana na mimi walikua ni mwanafunzi mmoja anaitwa Joseph Paulo au Mbena kwa jina maarufu, naye nilikuja kuona hafui dafu kwangu hivyo sikuona cha kusoma aliponifungia baba chumbani kwake, bali nilitengeneza kijitabu cha picha na nilikua ni mchoraji mzuri wa picha. Nilikua nikisikia tu mlango unafunguliwa hapo nafungua harakaharaka daftari na kujifanya nasoma sana kumbe nachora picha za watu, magari, nyumba na mambo tofautitofauti. Ikifika kesho darasani cha kwanza kama hamna mwalimu ilikua ni kuwaonesha marafiki zangu nimechora nini ambacho ni kipya na hapo naibuka na sifa nyingi “yaani wewe ni noma kwa kuchora”
Siku moja nilikatazwa na mwalimu wa madrasa kuchora picha za binadamu na wanyama. Hapo nikaogopa sana na kuanza kuchora vitu visivyokua hivyo. Wapo jamaa zangu waliniambia ziku ya kiama utakuja kuambiwa na Mwenyezi Mungu “haya vipulizie roho zao sasa viwe hai” nilijua yakini kua sina uwezo huo hivyo khofu ilinizidi na nikaachana na habari hiyo ila inapotokea tumechorewa darasani nikawa sina jinsi. Kipaji change cha kuchora kilikuja kunipa shida mbeleni kwani sikujua thamni ya na kipaji hicho ukizingatia ndoto zangu zilikua ni Udaktari. Yaani nilitamani siku moja niwe nipo chumba cha daktari nikiwa nimevaa kile kipimo chao cha kuweka kifuani au kwenye moyo na huku nimeva glaves kwa ajili ya kushughulikia upasuaji wa mioyo ya watu. Sikua mwoha hata kidogo kuona damu ikimiminika kwa kuchinjwa mnyama, ndege au mtu akiumia. Bali nilitamani niwe ndio mhudumu wa hayo.
Wakati tupo darasa la sita alikuja kaka yangu Yasini kutoka Dar es Salaam, naye ni mtoto wa baba mkubwa aliyeitwa Ahmadi, imamu msaidizi wa msikiti wa Makukula Buguruni jijini Dar es Salaam. Kaka Yasini alikuja kijijini kwa lengo la kusoma kuanzia darasa la sita mpaka kumaliza la saba. Hivyo nikawa naye katika masomo na ilipofika likizo tulisafiri pamoja kwenda Dar es Salaam kwa mwezi mmoja. Katika likizo hiyo nilikutana na rafiki mzuri jina lake Mussa ambaye asili yake ni Mkoa wa Tanga wilaya ya Lushoto Jimbo la Mtae goka. Kwa marafiki wangu wa kitanzania sijawahi kua na rafiki tuliyependana kama Mussa kwani mpaka familia yangu iliungana na yake kwa kule kutembeleana kwetu na hatimaye mwaka 2018 alioa mmoja wa madada wa familia zetu na hapo bwana mussa akawa ni shemeji yangu kwa dada yangu.
Baada ya kumaliza darasa la saba na matokeo yakaja vizuri, nilichaguliwa kusoma Iyunga Technical Secondary School ambapo nilianza kidato cha kwanza mwaka 2009. Shule hii ipo mkoa wa mbeya unaopakana na nchi za Malawi na Zambia. Nilisoma hapo miaka minne na nilichagua fani ya ziada ya ufundi wa kuchomelea vyuma (Welding and Metal Fabrication). Fani hii niliichagua kwa sababu lazima kila mwanafunzi afanye masomo ya ufundi lakini fani ya maisha yangu ilikua ni ileile ya udaktari.
Kwa mawazo yangu nilijiona nitakua wa kwanza katika darasa kwani nilijiamini kwakua nilikua wa kwanza kila mara nilipokua shule ya msingi. Kwa bahati mbaya jaribio (test) la kwanza lilikua ni somo la Technical drawing ambalo nilipata sifuri ‘0’ jambo ambalo lilinipa changamoto isiyo ya kawaida. Nikajipanga na kuja kupata ‘C’ ya 45 kwa jaribio lililofuata. Kasha baada ya hapo ikawa somo hilo ndilo pekee ninalofaulu kuliko mengine yote. Nilipata ‘A’ ya 90 na 95. Ufaulu wangu ulimpelekea baba kutafuta kujua kutoka kwa wanafunzi wa sekondari kua ni ni somo la aina gani hilo kwani alikua akitembea na karatasi yenye jina la “Technical Drwing” kila alipotumiwa matokeo yangu kutoka shuleni. Baada ya mwaka mmoja somo hili likabadilika na kuitwa mechanical Drafting ambapo ugumu wake uliongezeka zaidi. Kwa mtu yeyote aliyesoma shule ya ufundi anajua changamoto za masomo ya ufundi.
Baada ya changamoto za awali sasa ufaulu wangu ukawa ni wa wastani. Nikaendelea hivyo mpaka namaliza kidato cha nne. Kabla ya mtihani wa kidato cha nne marafiki zangu walinishauri sana niachane na habari za udaktari na nisome ufundi wa Architecture kwani waliona nilivyokua mtundu wa kuchora majengo na ramani mbalimbali za nyumba na wala sikua nikisoma ufundi huo. Nilikataa kila waliponishauri na kuwaambia kua mimi nataka kua Doctor na sio Engineer. Shule ya Iyunga ilikua karibu na chuo cha ufundi cha Mbeya Institute of Science and Technology MIST kilichokuja kubadilishwa jina na kuitwa Mbeya University of Science and Technology (MUST). Wanafunzi waliosoma chuo hiki walinishauri pia kuachana na fani ya udaktari na kusoma Architecture kwani wakati nikiwa na uwezo wa kuwasomesha wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo MUST na hali mimi bado nipo kidato cha pili. Nilipata sifa za kuchora ramani na picha nzuri za nyumba na magari kupitia Program ya AutoCard iliyotumika kwenye Computer hivyo wanafunzi mpaka wa mwaka wa pili katika chuo cha MUST niliwasaidia kwa kiasi kidogo. Pamoja na yote waliniona niko vizuri kwa kipaji hicho lakini sikukubali ushauri wao na mwisho nikawaza tu kua hawa ni watu wazima na wananishauri kwa sababu za msingi, je niko sahihi kukataa?. Nilijikuta nikikubali kusomea Architecture hasa nilipojua kua miaka mitatu ya stashahada (diploma) ya ufundi huo ningeweza kuajiriwa na kuanza maisha yangu. Hapo nilitia nia ya kuoa wakati nipo mwaka wa pili pindi nitakapochaguliwa kusomea ufundi huo kwa sababu wapo walio oa.
Nilimaliza kidato cha nne mwaka 2012. Cha ajabu matokeo yalivyotoka nilifaulu sana masomo ya udaktari yaani mchepuo wa PCB na hapo nikaanza kuhisi kukosa nafasi ya chuo cha ufundi. Baada ya miezi kadhaa tukaletewa taarifa za kuchaguliwa kuendelea na msomo lakini bahati mbaya mimi nilichaguliwa shule ambayo sikuwahi kuisikia duniani toka kuzaliwa kwangu, nilipaswa kusoma kusoma kidato cha tano na cha sita katika shule hiyo.
Ilikua ni Ulayasi High School. Shule hii ilijaa wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita na ilikua mchanganyiko wa wanafunzi wa kike na wa kiume ambapo kidato cha kwanza mpaka cha nne walikaa Hostel na makwao na wanafunzi wa kidato cha tano na sita walikaa bweni (boarding). Ni shule iliyopo wilaya ya njombe Mkoa wa Iringa. Kipindi hicho Njombe ilikua haijawa mkoa rasmi ambapo ilikua ni mwaka 2013.
Sikuweza kuvumilia kukaa katika shule ya Ulayasi kwani sikuzowea kusoma na wasichana katika ukubwa wangu, kumbuka kidato cha kwanza mpaka cha nne nimesoma shule ya wavulana tu. Pia hali ya hewa nayo ilikua ni baridi sana, hivyo kwa sababu hizo nihama baada tu ya miezi miwili katika shule hiyo.
Ndoto za kuoa zilihama nikaanza kufikiria nioe baada tu ya kumaliza kidato cha sita, kumbuka kwetu ni kawaida vijana wa kiume kuoa wakiwa na miaka ishirini au hata chini ya hapo.
Baba alikuja shuleni Ulayasi katika harakati za kunihamisha na tulibahatika kupata nafasi katika shule ya Azania High School ambayo ilikua ni ya wavulana tu na hapo ilitulia nafsi yangu. Kiukweli niliona taabu sana kusoma katika mchanganyiko wanaume na wanawake. Shule hii ya Azania ambayo ipo jijini Dar Es Salaam maeneo ya hospitali kuu ya taifa ya Muhimbili, nayo ilikua na wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita. Changamoto iliyonipata baada ya kuhamia Azania ni kua kule nilikotoka Ulayasi High School kulikua na shida ya walimu kwani walimuwengi walihama kutokana na hali ya hewa na uhaba wa huduma za kijamii. Baada ya kuingia Azania High School nilikuta baadhi ya masomo walimu ni wawiliwawili na walikua wameshapiga hatua kubwa sana. Nilianza kuhangaika kusoma kwa bidii bila kuwafikia wenzangu.
Kabla sijaingia kidato cha sita nilianza kusumbuliwa na kichwa hali iliyonifanya nianze kuzorota kimasomo. Nilishindwa kusoma baadhi ya nyakati kwani kichwa kiliuma pasi na kuelewa dawa ya aina yeyote. Baada ya kufanyiwa vipimo katika hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam ikagundulika kua tatizo ni macho ambapo nilipewa miwani ya kichwa, nayo ni miwani inayopunguza ukali wa mionzi ya mwanga hasa wa jua.
Nilipata nafuu na kupambana na masomo mpaka kumaliza kidato cha sita.
Katika Mahafali yangu ya kumaliza kidato cha sita, Mama (Bisurah), Mama mdogo (Samimu na Sikuzani na Mume wake), Mamamkwe, Bibi (Asiatu), Shangazi (Jamilah na Mume wake), Mdogoangu (Khalfan), Dada (Ashirunah na mwanawe wa kwanza) na jamaa zangu wengine walikuja kunifariji kwani hiyo safari haikua ndogo katika kipindi chote hicho cha miaka sita ya sekondari. Walinipa zawadi mbalimbali ambazo pesa tasilimu zilikua shilingi elfu sabini na mavazi tofautitofauti. Kwaweli nilihisi kupendwa sana na hizi familia na nilifurahia uwepo wao mpaka sasa ambapo naandika historia hii ya maisha yangu.
Kwa kurudi nyuma kidogo, wakati nilipomaliza kidato cha nne na kusubiria matokeo, nikawa nafundika watoto wa nyumbani na wa majirani ambapo walikuepo wanafunzi wa kidato cha tatu kutoka kijijini waliokuja likizo Dar Es Salaam. Miongoni mwao yupo ambaye alikuja kua mchumbaangu kabla sijamaliza kidato cha sita. Kumbuka baada ya kuanza kidato cha tano niliweka nia ya kuoa nikimaliza tu kidato cha sita. Nilikua na msimamo sana na jambo la kuoa japo wazee wangu hawakujua, kwani sikutaka kufikwa na maradhi ya uhuni na kupotea njia.
Binti huyo aliyeitwa Zainab (jina la nyumbani Zawadi) hakushiriki katika mahafali yangu kutokana na heshima ya kuwepo mamaake ambaye ni mkwe wangu mtarajiwa. Baada ya Mahafali kuisha nilimpa Zawadi zangu mamamkwe ampelekee Mchumbaangu mwanae ambaye hakupata ruhusa ya kuhudhuria mahafali hiyo. Hazikua zawadi kubwa, bali ni za kiuwanafunzi tu vikiwemo viatu, pochi ya kisasa na vitu vingine vidogovidogo. Zawadi ilifurahiwa sana mpaka nikajipa moyo kua sitokosa kumuoa binti Yule aliyemaliza kidato cha nne name nikiwa namaliza kidato cha sita.
Baada ya kumaliza kidato cha sita na kupata matokeo mazuri, niliomba chuo cha kikuu cha Dodoma (UDOM) na kukubaliwa kusomea kozi ya afya inayoitwa Bachelor of Science in Health and information Sysytem, lakini kwa bahati nzuri nilipata udhamini wa kwenda kusoma katika nchi ya Uturuki ambapo niligairi kwenda kusoma UDOM.
Ndoto ya kuoa baada ya kumaliza kidato cha sita ikavurugika tena na hapo nikajiona sasa nitachelewa kuoa jambo ambalo sikulitaka kwenye maisha yangu.
Kusoma katika nchi ya uturuki kulikua ni miaka mitano ambapo mmoja ni wa kujifunza lugha ya kituruki. Baada ya kumuaga mchumbaangu wa halali na kumuuliza je atanisubiria kwa miaka mitano?, alinijibu kua hata miaka saba. Nilijua alinipenda sana name nilimpenda na mashahidi wa kupendana kwetu walikua ni mama zetu ambao walituonya na kutuusia tabia nzuri.
Katika harakati za kujiandaa na safari ya kwenda Uturuki kimasomo nilipatwa na changamoto nyingi sana. Mwanzo nilipoteza kiasi cha shilingi laki moja kwa kuidondosha katika choo nyumani kwa dadaangu mchikichini kariakoo.
Nikiwa ndani ya daladala za Gongolamboto-Kariakoo Niliibiwa dola ishirini na shilingi elfu kumi kwa thamani ya jumla ya shilingi elfu hamsini na tatu za kitanzania. Wakati huo nilikua na dola sitini katika mfuko mwingine ambazo zilisalimika. Dola sitini zilikua ni kwa ajili ya kukata viza ya Uturuki.
Katika kipindi hichohicho nilipoteza vyeti vyangu muhimu vyote vya masomo na vya utambulisho. Ni baada ya bwana mmoja kubeba bahasha yangu wakati tupo stationary maneneo ya Lumumba road Mnazi mmoja Dar Es Salaam, aliibeba akijua ni bahasha yake na kunifanya niumie kichwa ndani ya siku tatu kwani baada ya siku tatu yule bwana ndipo alirejesha bahasha ile bila kupotea hata kitu kimoja. Haya yote yalikua ni maandalizi ya safari ya kwenda bara la Ulaya nchi ya turuki.
TANZIA
Muda huu ikiwa ni saa saba kamili usiku, wakati naendelea na kazi yangu ya kuandika historia ya maisha yangu, Nimepata simu ya Msiba wa babu yangu mzaa baba aliyeumwa karibia mwaka mzima. Ameiaga dunia usiku huu wa tarehe 5-4-2019 na sasa ni muda wa kufikiria mazishi ya babu yangu.
TANZIA
Siku ambayo nilivifuata vyeti vyangu vilivyopatikana baada ya kupotea kwa siku tatu, nikajishauri sana kulala Kariakoo kwa dadaangu au nirudi kitunda, na mwisho niliamua kurudi navyo vyeti vyangu kitunda Gongolamboto ambako ndiko nyumbani kwa walezi wangu Baba mdogo na Mama mdogo. Kumbe huko njiani naenda kukutana na balaa linguine. Ni pale stendi ya magari iliyoitwa Gerezani karibu na kituo cha Mwendokasi, wakati napanda gari simu yangu ilichomolewa mfukoni mwa suruali bila mimi kujua na huku nukiwa na furaha ya kupata vyeti vyangu. Kitendo cha kuingia kwenye gari naangalia simu siioni, dada mmoja akaniambia nitaje namba yangu ili aipigie ile simu tumbaini mwizi. Baada ya kupiga ikaita na ikapokelewa bila mtu yeyote kuongea na kisha ikakatwa na tulivyopiga tena ikawa ishzimwa na haikupatikana tena. Cha huzuni zaidi ni kwamba mwizi wa simu alitumia laini zangu kutapeli watu na alifanikiwa kumtapeli mama mmoja na mwanae ambao ni watu w Magomeni Dar Es Salaam. Aliwatapeli kiasi cha shilingi laki moja. Nilipata huzuni baada ya kupigiwa simu na watu hawa waliotapeliwa kwani nilisajili upya (renew) laini zangu zile zilizopotea. Likapita hili na nikawa na huzuni za kupotelewa na pesa pamoja na simu. Wala sikua mshamba yaliponitokea haya bali jambo likiwa limepangwa likukute basi hata uwe mtu wa aina gani litakukuta tu.
Tarehe zilivyosgea na kuipata viza nilianza kujipanga kwa safari ambapo nauli alinipia babaagu zaidi ya dola 760. Kwakweli ilikua ni gharamakubwa sana. Nikabahatika kupanda ndege ya Turkish Airline ambapo ilitumia masaa 7 kutua nchini Uturuki. Tulianza safari saa tisa usiku siku ya Jumatano katika uwanja wa Mwalimu J.K.Nyerere International Airpot na kutua katika uwanja wa Ataturk Havalimani nchini Uturuki majira ya saa nne asubuhi siku ya alkhamis. Hii ilikua ni safari ya usiku na iliku ni mara yangu ya kwanza kupanda ndege kwani sikuwahi hata kuigusa au kuiona kwa karibu kiasi hicho.
Hata hivyo nilikua na ndoto ya kupanda ndege ya Qatar kwani nilikua nikifurahi sana kuona ndege za Qatar zikitua na kuinuka katika Airpot ya Dar Es Salaam. Hivyo nilitamani ningepanda Qatar Airline badala ya Turkish Airline.
Ndani ya ndege kuna vyakula na vinywaji vizuri sana. Tuliletewa chakula katika usiku huo wa saa tisa ndani ya ndege na nilishindwa kula baadhi ya vitu kwani sijawahi hata kuviona duniani tangu nizaliwe na wala sikuipenda ladha ya vyakula hivyo.
Nakumbuka ndege ilikua ni kubwa sana maana Dirisha la kulia kuna siti tatu na kushoto pia tatu halafu katikati nne yani kuna njia mbili za kupita. Nilishangaa kuona ukubwa huu wakati nimezoea kuona ni kitu kidogo tu hasa inapopaa angani.
Katika safari ya uturuki niliongzana na wanafunzi wenzangu wengine ambao wapo tuliosoma pamoja Azania High School japo wao walikua mcepuo wa PCM nami nilikua PCB. Nilikaa na Rafikiangu Haji maarufu kwa jina la Jembe, naye aliwahi kua Amiri katika shule ya Azania. Tuliingia uturuki siku ya Alkhamis saa nne asubuhi. Hapo kwa mara ya kwanza tulipanda treni ya umeme kutoka airpot ya Istanbul Turkey iliyoitwa Ataturk Havalimani ambapo huyo Ataturk ndiye Raisi wao wa kwanza hapo Ututruki. Tukapanda treni kwa namna ya kulipiwa kwa kadi maalumu kwenye mashine za malipo ya nauli. Mimi binafsi niliona mengi ni ya ajabu sana ila skuonesha ushamba wangu. Kutoka Airpot tukashuka sehemu moja inaitwa Shirin-Evler ambapo tuliingia pahala na kula chakula kizuri kilichoitwa Shawarma na matunda kama Zeytuni na Zabibu. Baadaye tulienda kupumzika na kesho yake tulipelekwa chuoni. Kilikua ni chuo cha Ipek tawi la lugha ya kituruki yaani “Ipeki Universitesi dili merkezi”.
Hapo tukatambulishwa na tulikutana na marafiki zetu wengine waliotoka Tanzania na nchi nyingine mbalimbali duniani. Baada ya kujuana kwa kiasi, tulirejea nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya kuja chuo rasmi siku ya jumatatu.
Hapo tulianza kusoma rasmi lugha ya kituruki, mwaimu wetu mkuu alikua akiitwa Ercan ambaye ni mtunzi wa vitabu vya kusomeshea lugha ya kituruki. Madarasa yalikua ya kisasa sana kwani tulitumia projectors na ubao aina ya SmartBoard unaoongozwa kwa computer. Viti vya madarasa vilikua kama vya maofisini maana vina matairi na vinazungukazunguka kama viti vya saluni. Tulifurahia maisha ya nchi ile barani ulaya tukiwa watu masikini tuliotoka umasikinini.
Nilikuja kua maarufu na kujulikana na zaidi kwa mwalimu wetu Ercan na wanafunzi wenzangu kwa sababu ya ucheshi, uchangamfu na tabia chanya nyingine zisizokua hizo. Nilisoma miezi miwili na hapo nikaanza kuuguaugua. Baada ya vipimo vingi vya kisasa katika hospitali tofautitofauti ilikutikana sina tatizo na kumbe tatizo lilijificha tu wala halikuonekana. Kifua kilinibana sana na kunikosesha amani. Nilipigwa X-ray na kufungwa mitambo yenye nyayanyaya mwili mzima lakini tatizo halikuonekana. Nikakaa kwa muda na badae hali ikazidi kua mbaya. Nikapelekwa Hospitali ya chuo kikuu cha Fatih (Fatih Universitesi Hastanesi). Hapo nilipigwa tena X-Ray na kupimwa kwa CT-Scanner na baadae Doctor alisema kuna uchafu katika pafu la kushoto ambao ulionekana kama vijidudu aina ya Bacteria waliovamia mfumo wa upumuaji katika mwili wangu. Kutokana na uchumi kua mdogo matibabu yalisimama na kusababisha tatizo kuzidi kua kubwa. Mara moja nilishikwa na homa kali jioni na kushindwa hata kusimama. Niliswali kwa kukaa na baada ya swala jamaa zangu walitafuta tax na kunipeleka hospitali ya Bayram-Pasha, kichwa kiliuma sana. Nikawekewa dawa kama drip na kupata huduma ya harakaharaka na nilipata nafuu. Tuliporudi nyumani nilikua ni mzima kabisa. Baada ya masiku machache homa za usiku ziliibuka na nikawa hata nikilala nashadia kabisa kwani hali ilikua ni mbaya na sikuamini kama naweza kuamka asubuhi mzima au naweza kufika jioni sijafa. Baada ya kurejeshwa tena Hospitali ya Bayram-Pasha nilipimwa na kukutwa Pafu la kusoto limejaa maji karibia lote. Kwakweli hali ilikua ni mbaya sana katika upumuaji na niliishiwa na nguvu nikawa na mwendo kama wa mzee na hali ni kijana wa miaka ishirini na moja. Hapo madaktari waniandikia kwenda hospitali ya Emergence ya Vifua tena kwa haraka sana. Ilikua inaitwa Yedigule Gowuz Hastanesi (Yaani hospitali ya vifua ya Yedigule). Ilikua mbali na nyumbani. Huko watu wote walivaa maski kwani wagonjwa wote hapo ni wa vifua tu. Nilifanyiwa operesheni ndogo kwa njia ya mashine ys sindano ili kutolewa maji yaliyopo kwenye mapafu kwa ajili ya vipimo zaidi. Operesheni ilihitaji saini za kufa au kupona ambapo marafiki zangu walionipeleka waliogopa sana name niliwatoa woga kwa kuwaambia nipo tayari kwa lolote kwani Napata tabu sana kwa hali niliyo nayo.
Operesheni ilifanyika na nikawa salama na madhara machache tu. Baada ya vipimo juu ya maji yaliyotolewa ambayo yalikua ni nusu lita tu, tuliambiwa kua dozi ya kuyakausha maji yaliyopo ndani ya pafu ni dozi ya miezi sita au zaidi bila kupitiliza hata siku moja na iwe chini ya usimamizi wa daktari. Sikusita kutumia dozi hio ingawa niliogopa sana dawa na kupenda sindano nikisema “Bora sindano kumi kwangu kuliko kidonge kimoja cha paracetamol”.
Nilikaa Uturuki miezi mitatu bila kuendelea na masomo na huku nikitumikia dozi ya miezi sita. Baadae niliamua kurudi Tanzania nikiwa na dozi yangu na barua ya kitaifa ya kuendeleza dozi yangu nikiwa Tanzania. Ndoto za kuedelea na masomo nchini uturuki ziliishia hapo.
Nikarudi Tanzania na kuendelea na matibabu chini ya kituo cha matibabu kilichopo Posta Daresalaam (ADC) ambacho ni tawi la hospitali ya taifa ya Muhimbili. Nilimaliza matibabu na dozi za dawa na kupata nafuu kubwa ingawa mwili ulikua umeshaingia ubovu wa pafu moja la kushoto.
Mwaka wa kuugua na kutibiwa ukawa umepita na kikaja kipindi cha kuanza kuomba vyuo ambapo nilianza kuhangaika na sikupata tena chuo cha Dodoma “University of Dodoma (UDOM)” ambapo mwanzo nilichaguliwa kusoma fani ya afya iitwayo “Bachelor of Science in Health and Information System”. Hivyo nikaomba vyuo vingine na Hatimaye nikachaguliwa kujiunga na chuo cha Sumait “Sumait University” kilichopo Visiwani Zanzibar ndani ya kisiwa cha Unguja.
Baada ya kuchaguliwa chuo hiki nikajaribu kupanga upya mipango yangu iliyovurugika hapo awali na mpango wa kwanza kukaa sawa ukawa ni wa kuoa. Pasi na kumwambia mtu yeyote nikaanza rasmi kuchunguza mazingira kwa kila namna ili ikiwa yanastahiki kuishi na mke bila vikwazo nifanye haraka kuoa kabla elimu ya chuo haijanitawala. Kumbuka katika mambo niliyokua na ndoto nayo na kuzidisha dua zangu, yalikua ni Kuoa ndani ya miaka 25 au kabla hata haijafika, Kupanda ndege ya Qatar na Kuishi Zanzibar japo kwa mda mchache. Je ndoto hizi zinaweza kukamilika? Ndiyo, nyingine tayari mpaka sasa zimeshakamilika ikiwemo ya kupanda ndege ya Qatar, kwani katika safari ya kurudi kutoka uturuki ndio ndege nilizopanda tena mbili ambapo moja ilikua kutoka Uturuki kwenda Qatar na nyingine ilikua kutoka Qatar kwenda Dar-es-salaam Tanzania.
Basi baada ya kujipanga kifikra, nilipoingia tu chuoni mwaka wa kwanza nikaanza kuchunguza mazingira katika namna tatu kwa kujiuliza na kujijibu maswali haya: Je inawezekana kusoma na huku nimeoa? Je naweza kukaa na mke katika mazingira ya kichuo? Je nitakaa naye wapi? Haya yote niliyachunguza katika semista ya kwanza na pili, na semista ya tatu nikaanza kujikusanya kwa kuweka mipango madhubuti zaidi. Kumbuka kua mchumba ni yuleyule ambaye aliniahidi kuvumilia hata ikifika miaka saba ya masomo yangu. Alikua ni mwanamke muelewa na mwenye kujua lipi zuri linalofaa na lipi baya lisilofaa na alijiepusha sana na mambo ya anasa, alikua kaleleka katika ustaarabu wa hali ya juu yeye pekee katika familia yao na hakika alikua ndiye msichana pekee katika familia yao. Ni msichana mweupe mwenye kimo cha kati na kati, ana sura ya bashasha ya uchangamfu na mwenye aibu na adabu. Sikupata mwingine aliyenifaa zaidi yake naye aliitwa Zainab inagawa kwao walimwita Zawadi. Alinipenda mpaka nikahisi namkosesha amani. Kabla ya mitihani ya semista ya kwanza mwaka wa pili nikiwa chuoni nilianza kutangaza ndoa na marafiki zangu wa karibu hawakuamini kama kweli ninataka kuoa kwani waliniona mdogo kimwili na umri bila kujali kua akili zangu zilikua mbele zaidi ya jicho linapoishia kuona. Nilisafiri kwenda Dar-es-salaam wiki moja kabla ya siku ya ndoa na hatimaye ikafika ile tarehe ya ndoa. Ilikua ni siku ya jumapili tarehe 28/1/2019 majira ya alasiri ambapo nilikabidhiwa mke na kua mume wa mtu rasmi. Heshima yangu iliongezeka zaidi kwa kitendo hicho cha kujiunga na umoja wa maisha ya utulivu duniani, yaani kuoa. Ndoto yangu ya pili ilikamilikia hapo ambapo nilikua na miaka ishirini na nne wakati naingia ndoani. Nilifanya safari ya kurudi Zanzibar mimi na mke wangu mpenzi baada ya siku tatu za kukaa Dar-es-salaam toka siku ya ndoa. Ilikua ni siku ya jumatano majira ya saa tisa alasiri ambapo tulipanda boti ya Azam yaani Kilimanjaro Fast Ferries Boat na kuingia Zanzibar saa kumi na moja alasiri. Jambo ambalo sikutarajia baada ya kutoa begi mojamoja na kumwachia biharusi wakati naendelea kuchukua mabegi mengine na mizigo iliyobakia, mara nakuta ile ya mwanzo haipo. Nilipomuuliza biharusi wangu aliashiria kwa macho kunijulisha ni nani kachukua Begi la mwanzo. Kuinua macho yangu naona mbele kwa nje ya geti la bandarini kuna kundi kubwa la watu ambao ni wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Sumait wamekuja kunipokea. Nilihisi furaha na kufarijika ambako hakujawahi tokea katika hali kama ile. Sikuamini kua kuna watu wengi kiasi kile wanaowezakuja kuipokea harusi yangu. Walikuja na magari mawili, mimi nikaingia kwenye gari aina ya Noah pamoja na mke wangu. Baada ya kusalimiana na waliopanda ile Noah, nikawauliza kwanini mumenishtua kiasi kile? Mimi nilitegemea watakuja watu wachache tu na hii Noah watakaonishikia mabegi sasa naona mmekuja timu nzima! Wakanijibu kua mbona hapa tumekuja wachache sana! Tulikua ni wengi bali tulikosa basi letu la chuo ambalo ndilo tulilotaka kuja nalo kwahio hapa tumekuja wachache tu kwa sababu wengi walirudi. Yaani hapo ndio niliona ajabu zaidi kua pamoja na wingi wao ule kumbe wapo waliorudi.
Baada ya kufika nyumbani nlikokua nimepangisha ambapo nilikua mpangaji pekee, tulikaribishwa tena kana kwamba ni harusi mpya. Nilihisi raha kubwa sana ya kuoa kwa kushuhudia vile watu walivyonipokea. Nilianza rasmi maisha ya ndoa nikiwa kwangu kwakupanga na kuanza kuzoea taratibu mpaka leo hii tarehe 2/5/2019 jioni ya alkhamis kuamkia ijumaa ninapewa taarifa njema kua mke wangu Zainab kajifungua motto wa kiume katika hospitali ya Amana jijini Dar-es-salaam. Najihisi furaha nyingine kwa kuitwa Baba wa halali kwani nilijizuia sana na maovu hasa yale yanayopelekea kuitwa baba wa haramu. Tulimpa motto wetu jina la Haarith.
Tarehe 27 mwezi wa 7 mwaka 2019 nilimaliza rasmi mitihani ya chuo kikuu katika chuo cha kikuu cha SUMAIT hapa Zanzibar na tarehe 29 mwezi wa 8 mwaka huohuo matokeo ya mitihani yetu yalitoka ambapo nilipata Grading Point Average (GPA) ya 3.7 kwa matokeo ya semista ya mwisho. Nilifurahia kufaulu kwangu kwani si kazi ndogo niliyoifanya tangu chekehea mpaka chuo kikuu na kumaliza bila kufeli hata ngazi moja.
KUJIFUNZA UDEREVA
Katika moja ya ndoto zangu pia ilikua napenda kua dereva mzuri wa magari madogo na pikipiki. Nilijifunza pikipiki pasi na mwalimu na nilikua bado sijafika hata kidato cha nne. Baadae kabla ya kumaliza chuo nilianza kozi ya udereva katika Chuo cha udereva kiitwacho MAMBO 10 DRIVING SCHOOL kilicho ndani ya chuo cha ufundi cha Karume, KARUME INSTITUTE OF SCIENCE AND TECHNOLOGY (KIST) ZANZIBR. Lengo lilikua niwe na leseni ya halali ya udereva wa magri na pikipiki na nilifanikiwa katika hilo.


Comments
Post a Comment